TAFORI YAWASIHI WATANZANIA KUWEKEZA KWENYE MISITU

Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kupitia maonesho ya 47 ya kimataifa ya kibiashara, Sabasaba yanayoendelea jiini Dar es Salaam, imewasisitiza wadau wa misitu na ufugaji nyuki kuwekeza kibiashara kwa kuzingatia njia sahihi zilizofanyiwa utafiti. Akizungumza na baadhi ya wageni na wenyeji mbalimbali waliopata nafasi ya kutembelea banda la maonesho lililoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Afisa Ufugaji Nyuki Bw. Stanslauss Lukiko amewasisitiza wageni na wenyeji kutembelea banda la TAFORI ili kupata ushauri wa kitaalamu unaoambatana na taarifa ya utafiti juu ya ufugaji nyuki na upandaji miti kibiashara.