WARSHA YA MIKAKATI

Warsha hii ilikuwa ni warsha ya wadau ya kupitia rasimu mbalimbali za kuendeleza sekta ya misitu nchini. Rasimu za mikakati iliyopitiwa ni pamoja na Mkakati wa taifa wa kilimo misitu; Mkakati wa taifa wa kendeleza siti mbao; Mkakati wa kueneza kiongozi cha mafunzo ya chakula na msituni; na Mwongozo wa kuwezesha mashirika ya wakulima wa chakula na misitu kushiriki kwenye michakato ya sera. Warsha hii ilikuwa ni ya siku 2, Tarehe 17 – 18 Februari 2022 katika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania, Morogoro. Wadau waliohudhuria warsha hii ni TAFORI, BTI, FTI, FDT, TaFF, TFS, TFCG, ICRAF, FORVAC, WWF, TFNC, TARI, FITI, UDOM, MVIWAMA, LEAD Foundation, HUDEFO, MJUMITA, MVIWATA, SUA na FAO. Katika warsha hii Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara wa Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa. Katika warsha hii wadau waliweza kutoa mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha mikakati tajwa kwa maendeleo ya Taifa.