Photo gallery

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Dk. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Deusdedit Bwoyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI Dk. Revocatus Mushumbusi wakifanya ziara katika mabanda ya taasisi na wajasiriamali wanaotangaza huduma na bidhaa zinazotokana na mazao ya Nyuki kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kupata taarifa kutoka kwa Wataalamu katika siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani Mei 20, 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.
Mhe. Balozi Dk. Pindi Chana Waziri wa Maliasili na Utalii wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii katika Mwaka wa Fedha 2024/25, katika Kikao cha 27 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ,maadhimisho ya siku siku 4 kuanzia Mei 17 hadi 20, 2025
Mtaalamu wa Utafiti wa Ufugaji Nyuki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Bw. Stephen Msemo akifanya mawasilisho ya matokeo ya kitafiti kuhusu “Usimamizi wa Makundi ya Nyuki na Manzuki katika Kukuza Uchumi” kwa wadau, wakulima na wafugaji wa Nyuki, kwa ajili ya kuimarisha afya na kujikwamua kiuchumi ikiendana na kauli mbiu ya maadhimisho isemayo “Nyuki kwa Uhai na Uchumi Imara, Tuwahifadhi”. Mei 18, 2025 katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma,