Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim amezindua “Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki kwa Tanzania Iliyobora (Achia Shoka, Tundika Mzinga)”. Kwa lengo la kuongeza viwango vya uzalishaji wa asali kutoka tani 34, 861 hadi kufikia tani 75,000 ifikapo Juni 2035 na kuongeza mauzo ya mazao ya nyuki katika masoko ya kikanda na kimataifa, na kutoa rai kwa wadau wote watakao husika katika mpango hui kuutekeleza kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa ili kujenga imani kwa wananchi mmoja mmoja watao amua kuingia katika sekta hii.