
TAFORI ikiwakilishwa na Dkt. Chelestino Peter Balama (Mkurugenzi wa Utafiti wa Misitu, na Mjumbe wa Kamati ya Mimea ya CITES kutoka Afrika), imeshiriki Mkutano wa 78 wa Kamati Kuu ya Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora – CITES) uliofanyika tarehe 03 hadi 08 Februari, 2025 Jijini Geneva, Uswisi.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa, kulikuwa na ajenda zinazohusu biashara ya mazao ya misitu, hasa inayohusu Mapitio ya Biashara Muhimu kwa miti ya Mpingo na Msandari (Review of Significant Trade in specimens of Appendix-II species).
Mkutano huu ulikutanisha zaidi ya Washiriki 600, kutoka katika mataifa wanachama wa Mkataba wa CITES Bofya hapa kutazama zaidi….