Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Selemani Mkomi, leo ametembelea banda la TAFORI katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, Dodoma.
Katika ziara hiyo, amepata fursa ya kujionea huduma na taarifa za matokeo ya tafiti zinazotolewa na TAFORI kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta ya misitu na nyuki nchini.
#WikiYaUtumishiWaUmma2026 #TAFORI