NAIBU KATIBU MKUU WA UTALII, BW. MABULA AFANYA ZIARA TAFORI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aneshughulikia Masuala ya Utalii Bw. Nkoba Mabula amefanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na kupongeza taasisi kwa kufanya na kuratibu tafiti katika sekta ya Misitu na Nyuki nchini hasa tafiti zinazofanyika kwenye misitu ya hifadhi ya mazingira asilia, ambayo imeongeza fursa za Utalii Ikolojia.

Ametoa pongezi hizo hii leo Agosti 28, 2025, TAFORI Makao Makuu, baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Revocatus Mushumbusi na Mkurugenzi wa Utafiti Dk. Chelestino Balama kupitia kikao na Menejimenti ya Taasisi, kuhusu tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanywa na TAFORI katika Misitu na Ufugaji Nyuki haswa Tafiti za Utalii Ikolojia katika Milima ya Tao la Mashariki, ili kuona namna Serikali inavyoweza kunufaika na sekta hiyo katika kuongeza Pato la Taifa.

Aidha, ameipongeza Taasisi kwa uratibu mzuri wa tafiti zinazohusiana na majanga ya moto kwenye misitu ili ilikulinda na kurejesha uoto wa asili katika Misitu hiyo, ambayo ina fursa kubwa kwenye Utalii Ikolojia.