WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA AZINDUA MPANGO WA KUENDELEZA SEKTA YA UFUGAJI NYUKI KWA TANZANIA ILIYO BORA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim amezindua “Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki kwa Tanzania Iliyobora (Achia Shoka, Tundika Mzinga)”. Kwa lengo la kuongeza viwango vya uzalishaji wa asali kutoka tani 34, 861 hadi kufikia tani 75,000 ifikapo Juni 2035 na kuongeza mauzo ya mazao ya nyuki katika masoko ya kikanda na kimataifa, na kutoa rai kwa wadau wote watakao husika katika mpango hui kuutekeleza kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa ili kujenga imani kwa wananchi mmoja mmoja watao amua kuingia katika sekta hii.

Uzinduzi huu umefanyika leo Mei 20, 2025 wakati Waziri Mkuu Mhe. Mjaliwa akihutubia wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani chini ya kauli mbiu isemayo “Nyuki kwa Uhain a Uchumi Imara, Tuwahifadhi” katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.