SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA WATAALAMU KUMI (10) WA MISITU KUTOKA CHUO KIKUU CHA ST. PETERSBURG, RUSSIA

Serikali ya Tanzania imewapokea wataalamu 10 kutoka Chuo Kikuu cha St. Petersburg, Russia 🇷🇺, waliowasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya kubadilishana ujuzi na teknolojia katika sekta ya misitu. Ziara hii ni sehemu ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Russia katika uhifadhi wa misitu na maendeleo ya sekta hiyo.

Ushirikiano huu ulianza kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu baada ya kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika na Russia mwaka 2023. Kwa muktadha huo, taasisi za TFS, TAFORI, na SUA zimehusika katika maandalizi ya makubaliano haya, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kiutafiti kati ya nchi hizi mbili.

Katika utaratibu wa kubadilishana wataalamu, Tanzania pia itatuma wataalamu wake 10 kwenda Russia mwezi Mei 2025. Wataalamu hawa wa Russia wataendelea na ziara yao nchini kuanzia Machi 9 hadi 16.